Rangers kushuka dimbani kesho

rangers
Mwandishi Wetu
LIGI Daraja la kwanza inaendelea kesho kwa michezo miwili huku timu ya Friends Rangers ikishuka kwenye Uwanja wa mabatini Mlandizi kuvaana na timu ya KMC.
Ofisa Habari wa klabu ya Friends Rangers, Asha Kigundula, alisema kuwa wanatambua ugumu wa
mechi hiyo lakini lengo lao ni kushinda na kupata pointi tatu.
Kigundula alisema anatambua kama wapinzani wao wamejipanga kushinda, lakini nao wapo kwa lengo la kufanya vizuri na kuondoka na pointi tatu.
Alisema wao hawajataka tamaa wana amini bado wana nafasi ya kupigania kupanda daraja na kucheza ligi kuu msimu ujao.
“Mechi ngumu sana lakini tumejipanga kushinda mchezo wetu huu, tunatambua uzuri wa KMC lakini nasi tuko vizuri kama tulivyowatoa kwenye michuano ya FA Cup.
Alisema kuwa wapo katika nafasi nzuri ya kupigana na kufanikiwa kuvuka vizingiti wanavyowekewa na baadhi ya wadau wengi.
Wakati huo huo mechi nyingine ya ligi hiyo itakuwa kati ya Africa Lyon dhidi ya Kiluvya United mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Karume.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment