Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko akifafanua kwa waandishi wa
Habari (hawapo pichani) kuhusu namna mfumo mpya wa kuhakiki taarifa za
umiliki wa viwanja na mashamba kwa kutumia simu za mkononi
utakakavyofanya kazi na kusaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya
ardhi hapa nchini,kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TEHAMA
Bw.Alexander Karaba.
………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi
Serikali yaanza kutumia mfumo wa
simu za mkononi kuwawezesha wamiliki wa ardhi kuhakiki na kuboresha
taarifa zao za ardhi kote nchini.
Hayo yamesemwa jijini Dar es
salaam na Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi
Mboza Luandiko wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga
kutambulisha huduma hiyo mpya kwa wananchi.
“Mfumo huu unamwezesha mmiliki wa
ardhi kuhakiki na kuboresha taarifa zake za ardhi kwa kutumia simu yake
ya mkononi kwa kuandika neno Ardhi kwenda namba 15774” alisisitiza
Luandiko
Akifafanua Luandiko amesema kuwa
wakati mwananchi anatuma ujumbe huo anatakiwa awea na nyaraka zake za
umiliki wa ardhi au barua ya toleo kwa wale ambao bado hawajapata hati.
Akizungumzia faida za mfumo huo
Luandiko amebainisha kuwa utasaidia kulinda milki za wateja na kuondoa
kabisa tatizo la matapeli.
Faida nyingine ni kuongeza uwazi
katika kugawa ardhi na hivyo kupunguza migogoro ya ardhi ambapo hati
milki zitatolewa kwa wingi zaidi kwa kuwa mfumo huo ni rafiki katika
utoaji wa huduma.
Aidha mfumo huu utarahisisha
Mawasiliano kati ya mmiliki wa ardhi na Wizara hali itakayoongeza tija
katika upatikanaji wa huduma kwa kuwa zinaweza kupatikana kwa njia ya
simu ya mkononi ikilinganishwa na hapo awali ambapo mwananchi alitakiwa
kufika katika Ofisi za Wizara ili kupata huduma husika.
Huduma ya mfumo wa uhakiki wa
taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba imeanza katika mkoa wa Dar es
salaam na baada ya hapo tathmini itafanyika kabla ya kuanza kutumika
katika Mikoa yote.
0 comments :
Post a Comment