Kesi Ya Kamanda Godfrey Nzowa Dhidi Ya Kamanda Suleiman Kova Kuunguruma Leo

Nkupamah Media:


Kesi ya maofisa wawili waandamizi wa polisi kutaka kuuziwa nyumba ya Serikali inaanza kunguruma leo katika kikao cha Mahakama ya Rufaa mjini Arusha.

Wanaopambana katika kesi hiyo ni Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa anayemshtaki kamanda mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufaa waliopo Arusha, Jaji Mbarouk Salum Mbarouk alisema juzi kuwa jumla ya kesi 50 zitaanza kusikilizwa wiki hii.

Alisema kati ya kesi zitakazosikilizwa, tisa ni za madai, 18 za jinai na 23 za maombi ya madai.

Mbali na Jaji Mabrouk, wengine wanaotarajiwa kusikiliza kesi hizo ni Jaji Musa Kipenka na Jaji Bernard Luanda.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment