Pluijm Anyemelea Singida United


TIMU ya Singida United imempa mkataba wa miaka miwili kiungo wa Chicken Inn ya Zimbabwe, Tafadzwa Kutinyu huku usajili wake ukisimamiwa na kocha wa zamani wa Yanga, Hans Pluijm anayetajwa kutua Singida muda wowote kuanzia sasa.
Pluijm amevunjiwa mkataba wake na mwajiri wake wa zamani Yanga kutokana na kile kilichoelezwa kuwa klabu hiyo inakabiliwa na ukata hivyo kushindwa kumudu kumlipa mshahara na gharama zingine.
Suala la Pluijm pamoja na usajili unaoendelea kwenye timu hiyo mpya katika ligi msimu ujao unasimamiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.
Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrahiman Sima alisema kuwa, “Bado tunaendelea na usajili ila Kutinyu tumemalizana naye na bado tunaendelea na wengine wa kigeni na wazawa.
“Suala la Pluijm litatolewa taarifa kama lipo ama halipo, maana ni mazungumzo ya awali yamefanywa ila hatuwezi kutamka kuwa ni kocha wetu wakati hatujamalizana naye litakuwa si jambo la busara,” alisema Sima.
Kuhusu mchakato wa wachezaji wazawa Sima alisema kuwa, “Tutaangalia taarifa na uhitaji wa benchi la ufundi hapo baadaye, muda wa kufunguliwa kwa usajili wetu bado,”.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment