Heri ya mwaka mpya. Nina
furaha kuwafahamisha kuwa kitabu kipya, “Dokta John Pombe Magufuli:
Safari ya Urais, Mafaniko na Changamoto katika Urais wake” sasa
kinapatikana. Kitabu hiki ni mfululizo wa vitabu kadhaa ninavyotarajia
kuvichapisha mwaka huu 2016.
Wakati kitabu hiki kikiingia
sokoni, kitabu kingine kuhusu taaluluma ya Usalama wa Taifa kipo katika
hatua za mwisho, na matarajio ni kukiingiza sokoni mwishoni mwa mwezi
huu.
Kitabu hiki cha Dokta Magufuli
kina sura sita. Katika utangulizi, kitabu kinazungumzia mazingira ya
uchaguzi mkuu uliopita, msisitizo ukiwa kwenye hali ya nchi ilivyokuwa
kabla ya uchaguzi huo.
Kadhalika, utangulizi huo
unaelezea mabadiliko ya ghalfa ya kisiasa, hususan ndani ya CCM,
yaliyojitokeza kufuatia jina la mwanasiasa aliyekuwa maarufu kuliko wote
wakati huo, Edward Lowassa, kukatwa na chama hicho tawala wakati wa
mchakato wa kupata mgombea wake wa kiti cha urais.
Sura ya kwanza inamtambulisha
Dokta Magufuli, kwa kuangalia historia fupi ya maisha yake. Sura ya pili
inaeleza mchakato aliopitia Dkt Magufuli hadi kuibuka mgombea wa urais
kwa tiketi ya CCM. Sura hii inachambua kwa undani ushindani miongoni mwa
makada zaidi ya 40 waliochukua fomu kuwania urais kupitia chama hicho.
Sura ya tatu inaelezea fursa
alizokuwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla katika kipindi cha kampeni na
uchaguzi mzima kwa ujumla. Sura hii inachambua uimara wa mwanasiasa
huyo sambamba na turufu za kawaida za CCM katika kila uchaguzi. Kwa
uapnde mwingine sura hiyo yaangalia pia mapungufu yaliyopelekea urahisi
kwa Dokta Magufuli kumshinda mpinzani wake mkuu Lowassa, sambamba na
mapungufu ya UKAWA yaliyoiwezesha CCM kushinda.
Sura ya nne inajadili
changamoto na vikwazo kwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla wakati wa
kampeni. Kadhalika, sura hii inazungumzia jinsi Lowassa na UKAWA
walivyoshindwa kutumia changamoto hizo za wapinzani wao.
Sura ya tano inajadili urais wa
Dokta Magufuli tangu aingie Ikulu, wakati sura ya mwisho inajadili
changamoto zinazoukabili urais wake na kutoa mapendekezo.
Nimejitahidi kadri nilivyoweza
kuandika kitabu hicho kama mtu niliyeufuatilia uchaguzi huo kwa karibu.
Natambua kuna wanaoweza kuwa na hofu kuwa ‘niliisapoti CCM na Dokta
Magufuli wakati wa kampeni, na kutoiunga mkono UKAWA na Lowassa.’ Naomba
kuwatoa hofu kwani kitabu hiki ni si cha kiitikadi bali kwa ajili ya
Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi.
UTAKIPATAJE?
Bei ya kitabu sasa ni Shilingi
4,000 tu. Ili kukipata, nunua kwa M-PESA namba 0744-313-200 jina JOHN
ZABLON MPEFO au TIGO-PESA namba 0652-112-071 jina CHRISTINE JOHN MANONGI
KARIBUNI SANA



0 comments :
Post a Comment