Shirikisho la Mpira wa Miguu
(TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa kocha msaidizi wa Taifa Stars
Hemed Suleiman “Morocco” kufutia kifo cha baba yake mzazi Suleiman Ally
Hemed
kilichotokea juzi kisiwani Zanzibar.
Katika salamu hizo za rambirambi,
TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wapo pamoja
na familia ya marheemu katika kipindi hiki kigumu cha maombeloezo.
Aidha pia TFF imetuma rambirambi
(ubani) wa shilingi laki mbili (200,000) kwa familia ya kocha Hemed
Moroco kufuatia kifo cha baba yake Suleiman Ally.
Mazishi ya marehmu Suleiman Ally Hemed mefanyika jana jioni mjini Zanzibar
0 comments :
Post a Comment