Viongozi wa ANC ni mafisadi'- Goldberg

Waondoeni viongozi wote wa ANC ni Mafisadi, asema Goldberg
Mwanaharakati maarufu wa Afrika Kusini, Denis Goldberg, ametoa wito kuwa viongozi wa chama
tawala cha ANC, waondoshwe madarakani.
Bwana Goldberg alifikishwa mahakamani pamoja na Nelson Mandela, na kutumikia kifungo cha miaka zaidi ya miaka 20 jela.
Lakin baada ya tathmini yake ya hali ya kisiasa ilivyo nchini Afrika Kusini, bwana Goldberg ameiambia idhaa ya BBC kuwa daraja zote za uongozi wa ANC, kutoka majimboni hadi ngazi za taifa, umehusika na rushwa.
 Goldberg anasema tamaa ya viongozi wa ngazi zote za ANC za kujilimbikizia mali inawanyima raia wa Afrika Kusini uhuru

Kigogo huyo wa kisiasa mwenye ushawishi mkubwa ,alisema lengo lao la kujitajirisha kwa haraka kumewanyima wa-Afrika Kusini uhuru wao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment