Baba yake Diamond: Nililia Sana Kutoalikwa Kwenye Arobaini ya Tiffah



Baba wa staa wa muziki Diamond Platnumz, Abdul Juma amesema hakuna siku alilia kwa uchungu kama siku ambayo mjukuu wake Tiffah alifanyiwa sherehe ya arobaini bila yeye kualikwa.
Akizungumza katika kipindi cha The Weekend Chat Show cha Clouds TV Jumamosi hii, Mzee Abdul alidai licha ya kuwa anawasiliana mara kwa mara na mama yake Diamond, lakini hakuwai kupewa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo mpaka alivyoona picha kwenye magazeti.
“Hakuna kitu kiliniuma kama kufanyiwa shughuli kwa yule dogo bila kualikwa.” Alisema Mzee Abdul.
“Yaani nakumbuka nilipigiwa simu nikaambiwa baba mwanao amepata mtoto lakini sio siku ya arobaini, niliumia sana, nililia, nililia sana kutoalikwa kwenye arobaini. Mimi nachoomba (Mama Diamond) asinisahau, kuna kazi nilifanya mpaka akawa hapo,” aliongeza.
Katika hatua nyingine mzee huyo amemtaka Diamond kufanya kazi kwa bidii.
“Mimi nampenda sana, kama kuna baya niliwatendea wanisamehe, mzazi akosehi, pia aendelee kujituma zaidi,” alisema Mzee Abdul

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment