Familia ya Diamond Platnumz yote ni brand, kwa mujibu wake mwenyewe.
Yuko sahihi kwasababu si yeye tu anayenufaika na ubalozi wa mabilioni ya shilingi wa Vodacom Tanzania. Mchumba wake Zari, mtoto wao Tiffah na mama yake Sandra, wote wamepiga mpunga kutokana na ubalozi huo unaoshuhudia familia nzima ikishiriki kwenye tangazo la promotion mpya ya mtandao huo, Ongea Deilee.
Ni mtu mmoja tu muhimu aliyekosekana – Abdul, baba yake Diamond ambaye kwa wengi anaonekana kuwa ‘mcharuko’ kiaina kiasi cha mwanae kutopenda kujihusisha naye. Bila shaka itamchukua miaka mingi Diamond kumtengeneza naye kuwa brand.
“The Most Powerful and Impactful Family in Africa!!!… Bibi Brand, Baba Brand, Mama Brand Mtoto ndio Usiseme!!…. thanks for the Big Love our People… and get ready for another Big Thing,” ameandika Diamond kwenye Instagram.
Kweli hela huenda kwa wenye nazo tayari!
0 comments :
Post a Comment