DOLA NUSU BILIONI ZILIZOPORWA NA BIN ALI ZAPATIKANA TUNISIA

nkupamah media Thursday, 11 February 2016


Dola nusu bilioni zilizoporwa na Bin Ali zapatikana Tunisia
Waziri wa Fedha wa Tunisia amesema kuwa nchi yake imefanikiwa kupata dola nusu bilioni kutokana na mauzo ya baadhi ya mali na milki zilizokuwa zimeporwa na dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Zainul Abidin bin Ali.
Salim Shakir amesema kuwa mamia ya milki na magari ya kifahari, vito vya dhahabu na almasi na kadhalika vilivyokuwa vikimilikiwa na dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Zainul Abidin bin Ali, familia na jamaa zake vilitwaliwa baada ya kiongozi huyo wa zamani
kukimbilia nchini Saudi Arabia kufuatia mapinduzi ya wananchi wa Tunisia mwaka 2011.
Waziri Shakir ameongeza kuwa tangu mwaka 2011 hadi sasa baadhi ya fedha hizo zimewekwa kwenye hazina ya serikali na nyingine zimetumiwa kulipa madeni ya Tunisia. Waziri wa Fedha wa Tunisia amesema fedha zilizopatikana kutokana na kuuza milki za dikteta za zamani wa nchi hiyo zimesaidia bajeti ya taifa na kupunguza haja ya serikali ya kujikopesha.
Serikali ya Tunsia inasema mali nyingi zilizokuwa zimeporwa na dikteta Zainul Abidin bin Ali bado hazijauzwa. Dikteta huyo amepewa hifadhi nchini Saudi Arabia.(VICTOR
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment