Michuano ya Kombe la Shirikisho
(Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuendelea wiki hii mzunguko wa
nne katika hatua ya 16 bora, kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja
mbalimbali nchini.
Jumatano Februari 24, 2016
kutakua na mchezo mmoja tu, ambapo timu ya Young Africans
watawakaribisha maafande wa JKT Mlale kutoka mkoani Ruvuma katika uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezwa majira ya saa 10:30
jioni.
Michezo miwili itachezwa siku ya
Ijumaa ambapo, Ndanda FC watakua wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa
Nagwanda Sijaon mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwakaribisha wakata
miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Jumamosi Februari 27, Mwadui FC
watawakaribisha maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui
Complex mjini Shinyanga, wakati jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza
dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo.
Mzunguko huo wa nne utakamilika
siku ya Jumapili ambapo, Simba SC watawakaribisha Singida United katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja
wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita
Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
NB: Rais wa TFF, Jamal Malinzi
kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi, ataongea na waandishi wa habari
katika Ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.


0 comments :
Post a Comment