- Kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 20 cha Sheria ya Kukuza Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999 pamoja na Kanuni zake kupitia Gazeti la Serikali 232 la tarehe 11Julai 2014, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu inakaribisha maombi ya kufanya shughuli za Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira kwa kipindi cha mwaka 2016.
- Waombaji wote wa Uwakala ni lazima wawe wamesajiliwa kama Kampuni ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira na watafanyakazi kwa mujibu na taratibu za matakwa ya sheria za nchi. Miongoni mwa majukumu yatakuwa ni pamoja na kuunganisha watafuta kazi na waajiri pasipo kuwa sehemu ya mahusiano ya kiajira yanayoweza kujitokeza baina ya watafuta kazi na Waajiri; na kutoa huduma zingine zinazohusiana na utafutaji kazi kama vile kutoa ushauri wa ajira na taarifa za soko la ajira kwa watafuta kazi na waajiri. Aidha, waombaji wa uwakala ni vema wakaainisha sekta wanazopenda kufanyia kazi kama Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira.
- Ifahamike kuwa kwa kusajiliwa kuwa Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira utaruhusiwa katika ukodishaji wa huduma (outsourcing of services) na siyo ukodishaji wa watu (outsourcing of persons) yaani kuajiri na kukodisha wafanyakazi, kuajiri kwa niaba ya kampuni nyingine, na kuwa sehemu ya mahusiano ya ajira ya Watafuta kazi na Waajiri
- Kampuni zinazoomba usajili zinatakiwa kusoma na kufahamu, kuelewa na kuzingatia Sheria ya Kukuza Huduma za Ajira Na. 9 ya 1999 na Kanuni zake. Kampuni zinatakiwa ziwasilishe maombi pamoja na nyaraka zifuatazo:
- Barua ya maombi;
- Katiba ya uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kampuni (Memorandum&Articles of Assocition).
- Hati ya usajili wa kampuni (Certificate of incorporation).
- Hati ya usajili wa Jina la Biashara (Business name)
- Leseni ya Biashara(Business License).
- Namba ya usajili wa mlipa kodi (Tax identification Number).
- Wasifu wa Kampuni au Wakala pamoja na ujuzi na uzoefu wa wataalamu katika uendeshaji wa huduma za ajira (Company profile).
- Uthibitisho wa Kampuni au Wakala katika kulipa kodi (The current tax clearance letter from Domestic revenue/larger tax payers department)
- Anuani kamili ya makazi (Permanent physical address) pamoja mkataba wa pango la ofisi
- Maombi yote ya usajili yawasilishwe ofisi ya Kamishna wa Kazi iliyopo jengo la Mwalimu Nyerere Pension Tower, Barabara ya Bibi Titi Mohamed, S.L.P. 1422, Dar es salaam.
- Aidha maombi haya yawasilishwe ndani ya wiki mbili tangu kutolewa kwa tangazo hili na yaambatane na ada ya usajili ya kipindi cha mwaka mmoja isiyorudishwa ya kiasi cha 500,000 (Laki tano tu).
Imetolewa na:
Kamishna wa Kazi
Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira, na Watu Wenye Walemavu.
29.02.2016
0 comments :
Post a Comment