Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya, (kushoto), akimpatia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni75 Kaimu mwenyekiti wa Saccos ya Ishimwe Kigoma Bi.Gabriela Hangula wakati wa hafla ya kukabidhi fedha kwa vikudi vya benki za vijijini (VICOBA), mkoani humo,. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. John Ndungulu,
Katibu Mtendaji wa Baraza la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Afisa
Mtendaji Mkuu, (CEO) wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba
Moshingi.Benki ya Posta imekabidhi jumla ya silingi milioni 175 kwa
vikundi hivyo viwili ikiwa ni mpango wa kuwawezesha wananchi kwa
kuwakooesha fedha kuinua mitaji yao chini ya udhamini wa baraza hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,
Issa Machibya (kushoto), akimpa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi
milioni 100 Mwenyekiti wa Saccos ya TWCC Kigoma, Dorothy Takwa. Wa pili
kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu,
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Bi.
Beng’ Issa na Afisa Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akishuhudia makabidhiano hayo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
Posta Sabasaba Moshingi akiongea na wana-saccos wa Manispaa ya
Kigoma-Ujiji, kabla ya kuwakabidhi kiasi cha fedha Shs milioni 175/=kama
mkopo ili kuinua mitaji yao. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kigoma, John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi
kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,
Issa Machibya
Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo wa
Benki ya Posta Tanzania, Henry Bwogi akimpa zawadi mmoja wa mwanachama
wa Saccos, kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki Tanzania,
Timotheo Mwakifulefule.
0 comments :
Post a Comment