Kaka wa Murtaza, Homayoun, mwenye Miaka 15, aliamua kumtengenezea Mdogo wake Jezi ya Argentina kutoka Mfuko wa Plastiki na kuiandika Jina la Messi na Namba 10 kwa Peni na kisha kuiposti Picha yake kwenye Mtandao wa Facebook Mwezi uliopita.
Picha hiyo ilizagaa mno Dunia nzima na kuwa maarufu kupindukia.
Sasa, Jorge Messi, Baba Mzazi wa Lionel Messi, amesema Lionel Messi anajua kuhusu Picha hizo na anataka kufanya kitu kwa ajili ya Shabiki wake huyo Mtoto wa Afghanistan ikiwa pamoja na kukutana nae.


0 comments :
Post a Comment