Hassan Almasi Kisabya Katibu Mkuu
wa Chama cha NRA Bara akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu ushiriki
wake katika uchaguzi wa marudia Zanzibar utakaofanyika Machi 20 mwaka
huu kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Leo jijini Dar es salaam ,
katikati ni Mussa Limamu Mketola Makamu Mwenyekiti Baraza la Wazee NRA
na kushoto ni Janken Malik Kasambara Afisa Habari wa Chama cha NRA. Nkupamah media:
…………………………………………………………………………………………………………
Na Nyakongo Manyama MAELEZO
Chama Cha National Reconstruction
Alliance (NRA) kutoka Zanzibar kimethibitisha kushiriki uchaguzi wa
marudio wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu baada ya
kikao kilichofanyika Februari 15.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu
Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa Chama hicho
kitashiriki uchaguzi wa marudio na kusisitiza kuwa tamko lililotolewa na
mgombea wao la kutoshiriki uchaguzi wa marudio lipuuzwe kwani ni tamko
lake binafsi na sio msimamo wa chama.
“Tamko lililotolewa tarehe
14/02/2016 Si Tamko la chama cha NRA bali ni tamko binafsi na wale
waliomuagiza kwani yeye hana mamlaka ya kukisemea chama wala wagombea
wengine wa chama pasipo Baraka na vikao halali vya chama” alisema
Kisabya.
Amesisitiza kuwa maamuzi ya
chama ni sharti yatoke katika chama na sio kwa mgombea na ikiwa yeye
amejitoa anatakiwa afuate taratibu za kisheria katika kujitoa kama
alivyofuata sheria katika kugombea nafasi hiyo.
Aidha, Chama kinatoa taarifa kwa
wagombea wote Zanzibar kujiandaa na wapiga kura kujitokeza kwa wingi
katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu ili
kutimiza haki yao kikatiba na kuchagua viongozi wao kwa kipindi cha
miaka mitano ijayo
Chama cha NRA ni miongoni mwa
vyama 14 vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka
jana katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofutwa kwa nafasi ya Rais.
0 comments :
Post a Comment