Profesa Muhongo: Sijawahi Kupokea Rushwa wala 10% Ya Mwekezaji

Nkupamah media:


WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema hajawahi kupokea rushwa kwa mtu yeyote wala asilimia 10 ya wawekezaji wa miradi mbalimbali ya umeme nchini.

Aidha, ametaka kuachwa kuingizwa kwa masuala ya siasa kwenye umeme, kwani umeme ni suala linalohitaji utaalamu zaidi na si maneno.

Alitoa kauli hizo juzi wakati akizungumza na wazalishaji wa umeme kwenye mkutano uliofanyika Mtera.

Mimi hakuna mtu yeyote dunia nzima aliyewahi kunipa rushwa, nia yangu ni kuhakikisha taifa linapata umeme ikiwa ni pamoja na kuongeza wawekezaji, sihitaji hela ya mtu,” alisema Profesa Muhongo.

Pia alisema baadhi ya mitandao ya kijamii, imekuwa ikiripoti kuwa amewaita wazalishaji hao ili wamlipe asilimia 10 ; na kusema jambo hilo si la kweli hata kidogo.

“Kwenye masuala mengine ya mtandao ambayo hayana ukweli wowote muwe mnajitetea,” alisema Profesa Muhongo. “Acheni kuingiza masuala ya siasa kwenye umeme,” alionya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment