STAND UNITED KUINGIA KAMBINI KATIKA MGODI WA DHAHABU BUZWAGI

nkupamah media:


images (3)
Timu ya Acacia Stand United fc (CHAMA LA WANA) inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Dhahabu ya ACACIA,mara baada ya kupoteza mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kufungwa goli 2-1 na  Simba Sc,kesho jumatatu inataraji kuingia kambini katika Mgodi wa Dhahabu BUZWAGI kujiandaa na mchezo wake unaofuata dhidi ya Maafande wa jeshi la kujenga taifa JKT Ruvu.
Afisa habari wa klabu hiyo ISAAC EDWARD amesema
kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba Sc ni sehemu ya matokeo ya Mpira wa miguu, kwani hivi sasa ligi ni ngumu na kila timu inapambana ili kupata matokeo mazuri.
“tumepoteza mchezo wetu tukiwa nyumbani dhidi ya Simba ni sehemu ya mchezo,tunajipanga na mchezo unaofata nyumbani ambao tutacheza na Jkt Ruvu , timu inataraji kuingia kambini siku ya kesho jumatatu katika Hosteli za Mgodi wa Dhahabu BUZWAGI kujiandaa na mchezo wetu unaofata”
Ameongeza kuwa mchezo ujao timu hiyo ya Acacia Stand United imejipanga kuhakikisha inapata ushindi ili wazidi kujiweka sehemu nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu  Tanzania Bara.
“Uongozi pamoja na Benchi la Ufundi tumejipanga vilivyo ili tupate pointi tatu ambazo zitazidi kutuweka katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi ”
Isaac amewaomba mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri nyumbani na Ugenini.
“ mashabiki wetu na wapenzi wa Acacia Stand United (Chama la wana) waendelee kuipa timu ushirikiano katika michezo yetu yote iliyobaki katika mzunguko wa pili ambao ni wa lala salama ikiwa tunacheza nyumbani na hata ugenini pia ”.
Acacia Stand United Fc kwasasa  imejikusanyia pointi 29 katika michezo yake 18 walioshuka dimbani katika msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment