Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) imeendelea kwa michezo miwili iliyopigwa jana Jumapili jioni.
Mchezo
uliovuta mashabiki wengi wa soka ni Manchester United iliyowakaribisha
Arsenal na mchezo huo kumalizika kwa wenyeji Man United kuibuka na
ushindi wa goli tatu kwa mbili.
Magoli
ya Man United yalifungwa na mchezaji chipukizi, Marcus Rashford katika
dakika ya 29 na 32 na baada ya magoli hayo Danny Welbeck aliifungia
Arsenal goli moja katika dakika ya 40 na kwenda pumziko wakiwa mbili kwa
moja.
Kipindi
cha pili Man United ilipata goli kupitia kwa Ander Herrera katika
dakika ya 65 na dakika ya 69, Mesut Ozili akaifungia Arsenal goli la
pili na mpaka mchezo unamalizika, Manchester United tatu na Arsenal
mbili.
Mchezo
mwingine ulikuwa kati ya Tottenham iliyokuwa mwenyeji wa Swansea City
na mchezo kumalizika kwa wenyeji Tottenham kuibuka na ushindi wa goli
mbili kwa moja.
Magoli
ya Tottenham yalifungwa na Nacer Chadli dakika ya 77 na Danny Rose
dakika ya 77, goli la Swansea lilifungwa na Alberto Paloschi dakika ya
19
0 comments :
Post a Comment