Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la
Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa
kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia
husika.
Dk.
Kigwangalla ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na msajili
wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine, ambapo katika tukio
hilo mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa mbalimbali
yaliyokwisha muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka
kama hilo.
Aidha,
Dk. Kigwangalla akitoa agizo la kufungwa kwa duka hilo, ameagiza
kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani mara moja il iwe fundishi
na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.
Kwa
upande wake, Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde amebainisha
kuwa, dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai kuuzwa katika maduka
hayo na pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia ni kinyume na
sharia kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya kutosha
kutoka kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa
binadamu n ahata kumsababishia matatizo.
Duka
hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche kutoka Hospitali ya Temeke, ni
miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu ambapo pia wachunguzi ha
wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi zaidi kinyume na ile
inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia mashaka
huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa milango
hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.
Dk.
Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi hilo la kukagua maduka ya dawa ni
la nchi nzima na watazunguka nchi nzima kufanya ukaguzi huo bila kutoa
taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha kinyume cha sharia
atachukuliwa hatua stahiki.
Mmoja wa maafisa wa TFDA, akikagua dawa katika duka hilo
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwaonyesha waandishi wa habari cheti
cha Famasia kilichoisha muda wake huku akiendelea na biashara yake hiyo
kinyume na sheria.
Baadhi
ya maafisa walioambatana na Naibu Waziri wa Afya. Dk Kigwangalla
wakimsikiliza kwa makini, Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa
tukio hilo.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akiongea kwa njia ya simu na mmiliki wa
duka hilo la Shine Pharmacy , Abraham Mathayo…ambaye alieleza kuwa yupo
Mkuranga, hivyo waliamua kuongea naye kwa njia ya simu kwa nini
anaendesha duka bila ya kutokuwa na vibali.
Mfamasia
Mkuu wa Serikali Henri Irunde, akitoa taarifa yake ya ukaguzi katika
duka hilo kwa wanahabari na Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo
pichani).
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo ya kufungwa kwa duka hilo
Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akitoka katika duka hilo la dawa baada ya kuagiza kulifunga..
0 comments :
Post a Comment