Nkupamah media::
Imeelezwa
kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya
ndoa za utotoni ambazo husabishwa na mila potufu, elimu duni na umaskini
unaopelekea wazazi kuwa na tamaa za kupata mali ili waweze kukidhi haja
zao pamoja na sheria kandamizi.
Kwa
mujibu wa takwimu kutoka Shirika la watu duniani (UNFPA) imeonyesha kuwa
Tanzania ni nchi ya tatu inayoongoza kwa ndoa za utotoni duniani kwa
kuwa na kiwango cha juu ukilinganisha na nchi zingine duniani.
Akielezea
kuhusu ripoti hiyo, ofisini kwake,Mwanasheria wa TAMWA Bi. Loyce Gondwe
alisema kuwa mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni ni Shinyanga,
Tabora, Mara, Dodoma, Lindi, Mbeya, Morogoro, Singida, Manyara, Mtwara,
Pwani, Arusha, Kilimanjaro, Kigoma, Dar Es salaam na Iringa.
Bi.Gondwe,
alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13
kimeruhusu mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 kuolewa kwa ridhaa ya
mahakama na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi na mtoto wa kiume aliyefikisha
umri wa miaka 18 anaweza kuoa.
Ameendelea
kusema kuwa licha ya kuwepo kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009,
inayotafsiri kwamba mtoto ni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18
bado sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inawaruhusu watoto wa kike chini ya
miaka 18 kuolewa na hivyo sheria ya ndoa kukinzana na sheria zingine.
Hata
hivyo, alisema licha ya Tanzania kuridhia mikataba mbalimbali ya
kimataifa inayopinga na kuzuia ndoa za utotoni, kama Mkataba wa Haki za
watoto wa mwaka 1989, ambao unamtafsiri mtoto kama yeyote mwenye umri
chini ya miaka 18 na Tamko la Haki za Binadamu ulimwenguni la mwaka
1948, Ibara ya 16(2) bado tatizo la ndoa za utotoni limeendelea kuwepo.
Naye
mratibu wa kituo cha usuluhishi TAMWA, Bi. Gladness Munuo alisema kuwa
ndoa za utotoni zina madhara mengi kwa mtoto ikiwemo kumyima haki yake
ya msingi ya kupata elimu na hivyo kumpotezea ndoto zake za kimaisha.
Bi. Munuo
alisema Ndoa za utotoni zinaweza kuleta madhara ya kiafya kwa mtoto
ikiwemo magonjwa ya fistula, ulemavu wa kudumu kwa sababu viungo haviko
tayari kushiriki tendo la ndoa na kushika mimba.
Aliendelea
kusema kuwa mtoto mdogo anapoingia kwenye ndoa anakumbana na changamoto
kubwa zingine za ndoa, kwa mfano migogoro ya ndoa kama vile kupigwa,
kufukuzwa, ulevi, utelekezwaji ambavyo hupelekea madhara makubwa kwa
mtoto katika maisha yake.
Hata
hivyo alitoa wito kwa serikali, jamii, watu binafsi na taasisi
mbalimbali kulinda haki za watoto ikiwemo kuchukua hatua ya kutoa
taarifa sehemu husika ili suala hilo liweze kuchukuliwa hatua na
kutatuliwa.
Imeandaliwa na Violeth Chonya(P.T)
0 comments :
Post a Comment