Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Atembelea Hospital ya Muhimbili Kukagua Utekelezaji wa Agizo la Rais Magufuli

Nkupamah media:

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimuametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli linatekelezwa mara moja.

Picha mbalimbali zinaonesha Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufulipamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment