Mchezaji wa timu ya Afya Sports Bara, Robert Ndimbe (kulia) Bara akiwania mpira na Saidi Bundara Zanzibar (kushoto) kutoka Afya Sports ya Zanzibar. Mchezo huo umefanyika leo kwenye Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. Afya Sports Bara 3-0 Afya Sports Zanzibar.
Mchezaji wa Afya Sports Zanzibar, Abdulheri Thani ( mwenye jezi namba tatu) akijaribu kufunga bao mbele ya kipa wa Afya Sports Bara, Salumu Saidi katika mchezo wa tamasha la pasaka. Mchezo huo umefanyika leo kwenye Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
…………………………………………………………………………………..
Timu ya Afya Sports Bara imeifunga timu ya Afya Sports Zanzibar mabao 3-0 katika mchezo uliyofanyika leo katika kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
Bao la kwanza limefungwa dakika ya 12 kipindi cha kwanza na mchezaji machachari kutoka Afya Bara, Ali magoma.
Katika kipindi cha pili Muhaji Kampala alitikisa nyavu na kufunga bao la pili, huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Ali Magoma.
Katika mchezo huo wachezaji wa Bara walionekana kuwa makini kulinda lango lao, huku morali ya wachezaji hao ikiwa juu katika kuhakikisha timu yao inaibuka na ushindi.
Kwa matokeo hayo timu ya Afya Sports Bara imeibuka kidedea ambapo mechi nyingine inatarajiwa kuchezwa Jumatatu.
Mchezo huo ni Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka kati ya Watumishi wa Sekta ya Afya Zanzibar na Watumishi wa Sekta ya Afya Bara kwa lengo la kuendeleza undugu na ushirikiano uliopo.
0 comments :
Post a Comment