Baada ya akaunti ya Belle 9 kuonekana kuandika ujumbe uliokuwa na maneno ya matusi kwa msanii mwenzake, Diamond Platnumz msanii huyo kutoka Moro amekanusha kuwa si yeye aliyeandika ujumbe huo.
Akiambatanisha na picha ya email ambayo ameipokea kutoka kwa uongozi wa Instagram Belle 9 aliandika kuwa “#SAMAqHANI NDUGU WATANZANIA KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA ,SAMAHANI SANA KWA MWANAMUZIKI MWENZANGU @diamondplatnumz #EMAIL MNAYOIONA HAPO JUU NDIO YA HACKER ALIEKUA ANAPOST NA KUTUKANA WATU ,TUNAENDA KUREPORT NA KAMA KUNA MTU ANAWEZA KUTUSAIDIA KUITRACK HII EMAIL TUNAMUOMBA MSAADA WAKE…..ASANTE SANA @kingkapita @kapitatechnologylimited KWA KUNISAIDIA KURUDISHA ACCOUNT YANGU #MUNGU AKUBARIKI #POLE SANA KWA NILIOWAKWAZA