Ikiwa zimeshapita siku 10 tangua kuachiwa hewani kwa video mpya ya wimbo wa #ShikaAdabuYako ya Msanii Ney wa Mitego, tayari wimbo huo umeanza kutamba kwenye vituo mbalimbali vya televisheni vya nje ikiwemo kituo cha Trace tv cha Ufaransa.
Akizungumza kwa njia ya simu na Modewjiblog, Ney wa Mitego amebainisha kuwa amejisikia faraja kubwa kwa wimbo wake kupigwa kwenye vituo hivyo vya nje ikiwemo kituo hicho cha trace tv.
“Kwa sasa ni furaha tu. Wimbo wangu wa ShikaAdabuYako unatamba kwenye vituo vingi vya nje ikiwemo Trace tv, Citizen tv na tv zote za Rwanda na Uganda wanapiga kila siku” ameeleza, Ney wa Mitego.
Aidha, Ney wa Mitego ameongeza kuwa, kesho 10 Machi 2016, anatarajia kuwa na mahojiano ya moja kwa moja (live) na moja ya kituo cha televisheni cha nchini Rwanda akiongelea wimbo huo wa #ShikaAdabuYako.
Pia ameongeza kuwa, tayari Mtv Base na vituo vingine wameomba wimbo huo na ameshawatumia na muda wowote wataendelea kurusha hewani.
Modewjiblog ilipotaka kujua kama vituo vya ndani (Bongo) vinaweza kuupiga wimbo huo, licha ya kuwa BASATA wao walifungia wimbo pekee yake (Audio), Ney ameeleza kuwa hakutaka sana kuusambaza katika vituo vya ndani zaidi kwa anayetaka kuucheza kwenye tv yake anayo ruhusa ya kuupakua kupitia mtandao wa You tube pekee ambapo hadi sasa kwenye mtadnao huo watu zaidi ya Laki nne wameweza ku-view wimbo huokwa ndani ya siku hizo 10, tokea alipo uachia humo.
Ney wa Mitego ameendelea kuwapongeza ‘fans’ wake kwa kuipokea vizuri video na wimbo huo kwani ndiyo wimbo pekee kwa mwaka huu ulioweza kuleta mapinduzi ikiwemo watu mbalimbali kuanza kumnyooshea vidole kutokana na ujumbe wa wimbo huo.
Unaweza kutazama hapa video hiyo:


0 comments :
Post a Comment