Amesema kuwa watashughulika na mmoja mmoja hasa waliobeba jina la watu wasiojulikana, kwa hiyo wananchi waendelee kuliaamini jeshi la polisi nchini wakati huu ambapo wanaendelea na kazi ya upelelezi ili kuwakamata waliohusika na mashambulio kwa Mbunge Tundu Lissu, Afisa mstaafu wa jeshi la wananchi na hakimu huko Mtwara kwani uchunguzi huo hauna ukomo mpaka wapatikane wote katika idadi yao waliohusika na mashambulizi.
Mwigulu ameyazungumza wataki akiongea na wananchi wa Kata ya Kinampanda Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, ambapo amesema kuwa kama yeye ndiye aliyepewa dhamana ya usalama wa raia na mali zao katika Wizara ya Mambo ya Ndani basi hapata tokea hata kitongoji kimoja uchochoro ambao utaonekana umeshindikana ndani ya nchi.



0 comments :
Post a Comment