
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema
hayo baada ya kukagua na kuridhika na ukarabati uliofanywa katika maeneo
ya Magulu, Munisagara, Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa.
“Hakikisheni
mnailinda reli hii kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko
vizuri na treni ya kwanza kutoka Dar Es Salam kwenda bara itapita na
kumaliza changamoto ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi
wanaotumiia reli hii”.Amesema Profesa Mbarawa.
Profesa
Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara,
Mzaganza, Kidete, Godegodena Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na
mafuriko ya mto Mkondoa kuacha Kilimo cha kuelekeza Maji kwenye reli
bali washirikiane na Serikali kudhibiti maji hayo kwenda kwenye hifadhi
ya reli.
Amesema
Shirika la Reli Tanzania ( TRL) linaendelea kuhakikisha kuwa treni
inayopita kwenye reli ya Kati inapata mzigo mwingi wa kusafirisha
kutoka bandarini za Tanga na Dar Es Salaam kuelekea mikoa ya Mwanza,
Kigoma na Mpanda, hivyo wafanyabiashara watumie fursa hiyo ili kupunguza
mzigo unaosafirishwa kwa Nadia ya barabara.
Waziri
Profesa Mbarawa ameteembelea bwawa la Kidete linaloelezwa kuwa chanzo
cha mafuriko pindi linapojaa wakati wa mvua za Vuli na Masika katika
mikoa ya Dodoma na Iringa.
0 comments :
Post a Comment