Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu yatembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya kamati ambapo Mo Blog imekuandalia habari picha za jinsi ziara hiyo ilivyokuwa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso (Mb), akisalimiana na uongozi wa Kampuni ya SMH Rail inayounda upya vichwa vya treni katika karakana ya reli iliyoko mkoani Morogoro, ambapo kamati hiyo iliyotembelea hivi karibuni kuona maendeleo ya uundwaji upya wa vichwa vya treni.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso (Mb) (wa pili kutoka kushoto), akipata maelezo ya namna kichwa kilichoundwa upya kinavyofanyakazi kutoka kwa mtaalam wa Kampuniya SMH Rail inayounda upya vichwa vya treni katika karakana ya reli iliyopo mkoani Morogoro, wakati kamati hiyo ilitembelea karakana hiyo hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi George Sambali, akitoa ufafanuzi wa namna Kiwanja cha Ndege cha Dodoma kinavyofanya kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati ilipotembelea kiwanja hicho hivi karibuni kuona namna kiwanja hicho kinavyofanya kazi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL ), Bw. Masanja Kadogosa. Akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati ilipotembelea stesheni ya Dodoma kuona utendaji wa shirika hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso (Mb), akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoaniTabora wakati walipotembelea barabara yaTabora-Nzega hivi karibuni.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza, Bw. Emmanuel Kaswanya, akitoa ufafanuzi wa namna bandari hiyo inavyofanyakazi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati ilipotembelea bandari hiyo.
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Kapteni Winton Mwassa, akiwasilisha ripoti ya utendaji wa Kampuni hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati ilipotembelea kampuni hiyo hivi karibuni.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso(Mb), akitoa maelekezo kwa Uongozi wa kampuni ya Huduma za Meli mara baada ya kupokea ripoti yao, wakati kamati hiyo ilipotembelea kampuni hiyo hivi karibuni.
0 comments :
Post a Comment