Nkupamah media:
Askari
Mlinzi kutoka Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza akiwa timamu kiulinzi
kama anavyoonekana katika eneo lake la kazi ili kuhakikisha Ulinzi na
Usalama wa Kambi hiyo Maalum iliyopo Mkoani Kagera.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja(katikati) akiongea na
Wakimbizi kutoka nchini Burundi(hawapo pichani) ambao wanahifadhiwa
katika Kambi hiyo Maalum kwa sababu za kiusalama.
Sehemu
ya kundi la ngo’mbe wa maziwa na nyama wakiwa zizini katika Shamba la
Mifugo linalomilikiwa na Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo
Kitengule lililopo Mkoani Kagera.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja akikagua ujenzi unaoendelea
wa Jengo la Banda la ndama katika Shamba la Mifugo linalomilikiwa na
Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo Kitengule lililopo Mkoani
Kagera alipotembelea katika ziara yake ya kikazi Machi 12, 2016.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa
Kambi ya Utenganisho Mwisa, SP. S. Lubinza alipotembelea katika Kambi
hiyo Machi 12, 2016 kisha kuongea na Wakimbizi kutoka Burundi ambao
wanazuiliwa katika Kambi hiyo kwa mujibu wa Sheria.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja pamoja na ujumbe wake
aliofuatana nao akikagua sehemu mbalimbali za Kambi hiyo ili kuona kama
zinakidhi viwango vinavyokubalika katika kuwahifadhi Wakimbizi hao ambao
wanahifadhiwa katika Kambi hiyo.
Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Mifugo linalomilikiwa na Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo Kitengule.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
0 comments :
Post a Comment