Nkupamah media:
Wajumbe wa mkutano mkuu wa
chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA,wilaya ya mbeya mjini
wamemtaka mwenyekiti wa chama hicho taifa,Fremman Mbowe kwenda haraka
jijini Mbeya kutatua mgogoro wa kiuongozi unaoendelea ndani ya chama
kabla haujaleta madhara makubwa na kusababisha chama hicho kupoteza
imani kwa wananchi.
Tamko la wajumbe hao wa
mkutano mkuu wa Chadema wilaya ya Mbeya mjini linatokana na kikao cha
ambacho kilifanyika hivi karibuni chini ya usimamizi wa makamu
mwenyekiti wa Chadema taifa upande wa Zanzibar,Mohamed Issa Mohamed
kilichoamua kuvunja kamati ya utendaji ya chama hicho wilaya ya Mbeya
mjini na kuweka uongozi wa muda, jambo ambalo linapingwa vikali na
wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho.
Kutokana na hatua hiyo
baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakadai kuwa wao hawautambui uongozi wa
muda uliowekwa na badala yake wataendelea kuwatambua viongozi
waliowachagua kikatiba.
Akitoa tamko la pamoja,
katibu wa mkutano huo,Hezron Edwin Mwaisengela amesema kuwa wajumbe
wanamtaka mwenyekiti wa chama taifa kufika mbeya haraka ili kutatua
mgogoro huo kwa maslahi mapana ya chama.
0 comments :
Post a Comment