Nkupamah media:
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.
Muhammed Jidawi akiwakaribisha washiriki wa Mkutano wa siku tatu wa
kutathmini sekta ya Afya Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach
Resort, Mazizini.
Kiongozi wa washirika wa
maendeleo kutoaka Mashiriki ya Umoja wa Mataifa DKT. Kirsten Havemann
akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya
Zanzibar unaofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Baadhi ya washirika wa maendeleo
na maafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano
huo uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua Mkutano wa 10 wa
kutathmini maendeleo ya sekta ya Afya Zanzibar kwa niaba ya Rais wa
Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizi nje kidogo ya
Mji wa Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar
Mahmoud Thabit Kombo akiteta jambo na kiongozi wa washirika wa maendeleo
kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Dkt. Kirsten Havemann wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar.
Mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi
na washiriki wa maendeleo na maafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar mara
baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku tatu wa kutathmini sekta ya
Afya unaofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
0 comments :
Post a Comment