Jeshi
la Polisi wilayani Mkalama, Mkoani Singida linamshikilia mkazi mmoja wa
Kijiji cha Iguguno, Tarafa ya Kinyangiri, maarufu kwa jina la
“Mwanaharakati”kwa tuhuma za kufanya vurugu kwenye mkutano wa mbunge wa
jimbo la Iramba mashariki(CCM), Allani Joseph Kiula.
Tukio
la kufanyika kwa vurugu hizo lilianza kujitokeza tangu mkutano huo
ulipoanza majira ya saa kumi jioni kwenye ofisi za afisa mtendaji wa
kata ya Iguguno ambapo idadi kubwa ya wananchi wa kijiji hicho pamoja na
vijiji vinavyokizunguka walihudhuria kumsikiliza mbunge wao aliyekwenda
kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao.
Hata
hivyo mwanaharakati huyo ambaye kwa muda mwingi alionekana kutoa kauli
za kejeli kwa mbunge huyo kwa sauti kali na ya juu,wakati wananchi
wakimsikiliza mwakilishi wao aliyewatembelea kwa mara ya kwanza
kuwashukuru na kusikiliza baadhi ya kero zinazowakabili.
Ilikuwa
ni muda wa saa 11:00 za jioni wakati ulipowadia muda wa maswali na
majibu kutoka kwa mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki, ndipo Muna
alipoinua mkono kuomba nafasi ya kuuliza maswali matatu kwa mbunge wao
huyo.
“Naitwa
Joseph Luther Muna “Mwanaharakati asante sana mwenyekiti, asante sana
mbunge na asante sana wageni mimi nina maswali matatu namshukuru sana
mbunge amesema kwamba mkutano wa kutatua kero…ndipo ghafla mbunge
alimtaka mwanaharakati huyo kuuliza swali badala ya kutoa maelezo marefu
kwa kuokoa muda,” alieleza shuhuda wa tukio hilo na kuongeza.
“Akawa
anazomewa na wananchi waliohudhuria mkutano huo, mwanaharakati huyo
alianza kwa swali la kwanza kwa kuuliza kuwa mkuu wa wilaya alikuja
tarehe 2, alipokuja alichukua kero 16 na siyo kero 20 kama unavyodai
wewe”
Katika
swali lake hilo Muna maarufu mwanaharakati aliweka wazi kuwa katika
hizo kero 16 na mbunge ni kero hivyo ni kwa nini asingesubiri kero hizo
zishughulikiwe na mkuu wa wilaya ili ijulikane zitatatuliwa vipi badala
ya yeye kusema anakwenda kuzishughulikia kero hizo.
Baada
ya maelezo yake hayo aliyokuwa akidai kuwa ni swali, wananchi kwa
pamoja waliohudhuria mkutano huo walijitokeza na kusisitiza kwamba Muna
hakuwa na swali la msingi zaidi ya ubabaishaji tu mkutanoni hapo na
waliendelea kumzomea kwa kitendo cha kupoteza nafasi kwa wengine
waliokuwa na maswali.
“Mheshimiwa mbunge ulipokwenda bungeni tangu uliporudi kutoka bungenihaujatupatia
mrejesho zaidi ya leo kusema kwamba unachomoa kero zako ili tuone kuwa
wewe huna kero unazotukwaza,kwa nini haujatupa mrejesho wa bungeni
kwanza ndipo uingie katika kutatua kero zetu,” alihoji mwanaharakati
huyo.
Hata baada ya kumaliza kuuliza
maswali hayo mwanaharakati huyo alianza kutoa lugha chafu kwa mbunge wa
jimbo hilo wakati aliposimama akijibu maswali ya wananchi,jambo
lililowafanya Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kumkamata na kumpeleka
kituoni kwa tuhuma za kufanya fujo mkutanoni.
Mtuhumiwa wa tuhuma hizo amewekwa katika kituo kidogo cha Polisi cha kata ya Iguguno akisubiri zaidi hatua za kisheria zaidi.
Na Jumbe Ismailly, Mkalama
Katibu
wa CCM wilaya ya Mkalama,Bi Ernestina (wa pili kutoka kushoto aliyevaa
fulana ya njano) akisikiliza kwa makini kero za wananchi wa kata ya
Iguguno wakati wa mkutano wa mbunge wa jimbo la Iramba mashariki(CCM),
Bwana Allani Kiula
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria mkutano wa mbuge wa jimbo la Iramba
mashariki(CCM)Bwana Allani Kiula alipokwenda kutoa shukurani kwa
wananchi hao pamoja na kupokea kero zao.
Askari
wa jeshi la polisi katika Kituo kidogo cha Mji mdogo wa
Iguguno(aliyevaa sare za jeshi la polisi) akiwa katika mkutano wa mbunge
wa jimbo la Iramba mashariki(CCM)Bwana Allani Kiula akisimamia ulinzi
katika kipindi chote cha mkutano na kuwachukulia hatua watu wenye nia ya
kuvuruga mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa mbuge wa jimbo la Iramba mashariki(CCM)Bwana Allani Kiula
0 comments :
Post a Comment