Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muunganao wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans (kushoto) wakati
alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa
Hospitali hiyo.Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya.
Mkurugenzi wa
Hospitali ya Walemavu CCBRT, Bi. Brenda Msangi akimueleza Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) kuhusu
namna ya utendaji kazi hospitalini hapo. Spika alitembelea hospitali
hiyo kuangalia utendaji kazi kama mlezi wao.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
(wa pili kulia) akipata maelekezo juu ya namna ya wagonjwa wa macho
wanavyowekewa macho bandia (artificial eyes) wakati alipotembelea
hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo.
Kulia ni ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya
nchini pamoja na Menejimenti ns Madaktari wa CCBRT alipowatembelea kama
mlezi wa Hospitali hiyo.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
(mwenye tai nyekundu) akipokea machapisho yanayohusu masuala ya walemavu
kutoka kwa Afisa Mtetezi CCBRT wa masuala ya walemavu, Bw. Fredrick
Msigala wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni
Mlezi wa Hospitali hiyo.


0 comments :
Post a Comment