Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.
Nyerembe Munasa Sabi akiongea na waandishi wa habari(Hawapo pichani)
kuhus harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari
Iyunga yaliyoteketea kwa moto hivi karibuni kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Jiji la Mbeya Bw.Dkt Samwel Lazaro.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.
Nyerembe Munasa Sabi akiongea na waandishi wa habari(Hawapo pichani)
kuhus harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari
Iyunga yaliyoteketea kwa moto hivi karibuni kulia ni Charles Mwakipesile
Mdau wa Maendeleo na kushoto ni Afisa Habari Idara ya Habari Raymond
Mushumbusi.
Picha zote na Beatrice Lyimo MAELEZO
……………………………………………………………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee itakafanyika kesho katika ukumbiwa
Ubungo Plaza kwa ajili ya kuchangia fedha zitakazowezesha kukarabati
mabweni manne ya shule ya Sekondari ya Ufundi ya Iyunga yaliyoungua hivi
karibuni.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Nyerembe
Munasa Sabi amesema kuwa wameamua kuomba nguvu kutoka kwa wadau wa elimu
na watanzania kwa ujumla kujumuika katika kuchangia shule ya sekondari
ya ufundi Iyunga ili waweze kukarabati mabweni yaliyoungua kwa moto.
“ Hadi sasa takribani wanafunzi
421 hawana mahala pa kulala kutokana na kuteketea kwa mabweni na kwa
kushirikiana na TAMISEMI tumeamua kusitiza masomo kuanzia tarehe11 March
hadi tarehe 01 Aprili ili kupisha ukarabati wa mabweni”
“ Tumeanza ujenzi wa baadhi ya
miundombinu iliyoteketea na mabweni ikiwa ni jitihada za wadau
mbalimbali waliochangia kutoka Mbeya na nawasihi wanambeya wale
waliosoma shule ya Iyunga na shule za Mbeya na watanzania kwa ujumka
kujitokeza kesho katika harambee hii” Alisema
Mhe. Nyerembe Munasa Sabi
aneongeza kuwa wamepokea michango mbalimbli kutoka kwa wadau wakiwemo
Mbeya Cement waliotoa mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya ujenzi na kwa
sasa mahitaji yaliyopo ni takribani Shillingi million 770 ili kukarabati
na kujenga majengo mapya kwa ajili ya shule hiyo.
Shule ya Sekondari ya Ufundi
Iyunga yenye wanafunzi takribani 9970 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha
sita imekumbwa na majanga ya moto ambayo yamesababisha athari kwa
watoto kutoendelea na masomo na uharibifu wa miundombinu ila Serikali
kupitia TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wamejipanga
kukusanya fedha kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa shule hiyo.


0 comments :
Post a Comment