Mchezaji wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya LA Galaxy ya Marekani, Steven Gerrard amejikuta njia panda baada ya kushindwa kufanya maamuzi ya hatma yake ya maisha ya soka.
Gerrard alitoa kali hiyo wakata akifanya mahojiano na Kampuni ya mavazi ya kiume, Mr Porter ambapo alionekana kushindwa kuelezea ni jambo gani anataraji kulifanya baada ya mkataba wake na LA Galaxy kumalizika mwaka huu mwishoni kama ataendelea kucheza mpira au kuwa kocha.
“Kwa muda huu bado nipo njia panda kujua nini tafanya labda tusubiri hadi mwisho wa msimu tutaona itakavyokuwa,
“Nina hakika mpaka Christmas nitakuwa katika nafasi ambayo takuwa nimeombwa kuifanya,” alisema Gerrard.
Aidha Gerrard alisema kuwa ana uhakika ataendelea kuwepo katika Ligi Kuu ya Marekani (MLS League) hata baada ya kumalizika kwa msimu huu.