Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa leo Machi 27.2016 imewadia kwa Watanzania kulishuhudia kwa mara ya kwanza tamasha kubwa na la Kimataifa la kumuimbia Mungu la Upendo Music Festival 2016, katika viwanja vya Leaders Club.
Tamasha hilo linaloandaliwa na kampuni ya Legendary Music Entertainment and Promotions Company Limited  wameweka bayana kuwa, wasanii na makundi ya muziki watapanda katika jukwaa la Kimataifa huku nyimbo zao hizo wakiimba ‘Live’ kwa kutumia vyombo yaani bendi, Miongoni mwa watakaomuimbia Mungu katika tamasha hilo ambao wana kalama na upeo mkubwa katika kusifu na kuabudu ni pamoja na: Angel Bernard, Emanuel Mbasha, Lynga George, Upendo Kihaile, Sarah Shilla, Faraja Ntaboba.
Pia wapo: Edson Mwasabwite, Angel Magoti, Abeid Ngosso, Ambwene Mwasongwe na Fridah Felix na wengine wengi wakiwemo Choir ya Kigogo KKKT, Gift and Beauty, Moses Saxer, Mise Ricprdias, The Joshua Generation, Glorious Worship Team, The Voice, Uinjilist Choir Kimara, Doxers Praise Team, Calvary Band, The Jordan, The Next level, Chang’ombe Vijana Choir, Uinjilist Kijitonyaama, Tumaini Shangilieni Choir na wengineo.
Aidha, katika viwanja hivyo vya LEADERS CLUB, Kinondoni,  kuanzia asubuhi kutakuwa na michezoo mbalimbali majira ya asubuhi ya saa nne ( 4:00) na kisha matukio mbalimbali ikiwemo michezo ya watoto huku wasanii hao mahiri katika kusifu na kumuimbia Mungu wakitarajia kuanza kupanda jukwaani majira ya mchana na kuendelea hadi usiku.
Pia kutakuwa na michezo ya Watoto na Uuzwaji wa biashara mbali mbali huku kiingilio kawaida ni Tsh. 5,000 na kwa viti maalum ni Tsh.10,000 huku kwa Watoto ni Tsh. 2,000.
“Music 100% Live, Njoo tumuimbie Mungu”.. Ulinzi na Usalama  ni wa hali ya juu nyoote munakaribiswa.
UpendoBaadhi ya waimbaji mahiri na wenye wito wa kumuimbia Mungu watakaokuwa katika tamasha hilo la Upendo Music Festivals 2016, leo Jumapili katika viwanja vya Leaders Club.