Kampeni ya TBL Group imezindua kampeni ya kuimarisha afya za wafanyakazi wake wote ambapo wanashiriki kufanya mazoezi ya mwili sambamba na kupatiwa kupatiwa elimu inayohusiana na lishe bora na matumizi ya vyakula visivyo na athari.
Afya Kwanza ambayo imeanzia kwa wafanyakazi waliopo Makao makuu na viwanda vilivyopo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imezinduliwa katika kiwanda cha Arusha na kushirikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Msimamizi wa Programu hii ,Julieth Mgani alisema kuwa itakuwa endelevu na wafanyakazi wameonekana kuifurahia katika kipindi cha muda mfupi tangia ianzishwe.
Wafanyakazi wa kiwanda cha TBL cha Arusha wakifanya mazoezi ya kukimbia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Afya Kwanza mwishoni mwa wiki.
Meneja Uendeshaji wa taasisi ya AAR Insurance Tanzania Ltd, Dk Harold Adamson akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha TBL mkoa wa Arusha juu ya umuhimu wa kuimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Afya Kwanza uliofanyika kiwandani hapo mwishoni mwa wiki.
Meneja wa kiwanda cha TBL mkoa wa Arusha,Meneja wa kiwanda cha TBL mkoa wa Arusha,Salvatory Rweyemamu akipiga mpira kuashiria kuanzishwa kwa kampeni ya Afya Kwanza iliyoanzishwa na TBL Group kwa lengo la kuimarisha afya za wafanyakazi wake. akipiga mpira kuashiria kuanzishwa kwa kampeni ya Afya Kwanza iliyoanzishwa na TBL Group kwa lengo la kuimarisha afya za wafanyakazi wake.
Mazoezi ya viungo yakiendelea.
Wafanyakazi wa TBL kiwanda cha Arusha wakimsikiliza mtaalamu wa lishe huku wakijipatia matunda baada ya kufanya mazoezi ya kuimarisha viungo vyao wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Afya Kwanza iliyofanyika kwenye kiwanda hicho eneo la Themi jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
0 comments :
Post a Comment