Ufisadi: Tajiri zaidi Iran ahukumiwa kifo

  • Nkupamah media:
Image captionTajiri zaidi Iran Babak Zanjani ahukumiwa kifo
Mfanyabiashara tajiri wa Iran, Babak Zanjani, amepatikana na hatia ya ufisadi, na kuhukumiwa kifo.
Bwana Zanjani alikamatwa mwaka wa 2013, baada ya kutuhumiwa kuwa alichukua dola bilioni moja nukta 9 za pato la taifa, kutokana na mafuta.
Alikanusha tuhuma hizo.
Image copyrightReuters
Image captionBabak Zanjani, amepatikana na hatia ya ufisadi, na kuhukumiwa kifo.
Bwana Zanjani alisusiwa na Marekani na Umoja wa Ulaya, kwa kuisaidia serikali ya Iran na makampuni kadha, kuhepa vikwazo vya kiuchumi vya wakati huo, dhidi ya mafuta kutoka Iran.
Alikiri kuwa alitumia makampuni kadha katika Umoja wa falme za Imarati, Uturuki na Malaysia, kuuza mamilioni ya mapipa ya mafuta ya Iran, kwa niaba ya serikali.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment