Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Ali Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 amemteua Mhe. Balozi Seif Ali Iddi kuwa makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar. Uteuzi huo umeanza leo tarehe jana 28, Machi 2016.
Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa usiku wa jana kutoka Visiwani Zanzibar, Imefafanua kuwa, Rais amemteua Balozi Seif Ali Idd kushika wadhaifa huo. Hii ni siku kadhaa kupita tokea alipoapishwa kuwa Rais wa Zanzibar.
Awali Balozi Seif Idd alikuwa anashikilia nafasi ya Umakamu wa Pili wa Rais Zanzibar wakati wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK).
IMG_8813Pichani ni Rais Dk. Shein akisalimiana na Balozi Seif Ali Idd. (Picha ya Maktaba).