Shirikisho la Mpira wa Miguu
barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya waamuzi watakaochezesha na
kusimamia michezo ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC), kuwania kufuzu kwa
Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) pamoja na kuwania kufuzu kwa Fainali
za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) mwaka 2017.
Michael Richard Wambura
ameteuliwa kuwa Kamisaa wa Mchezo Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF
CC) kati ya Al Shandy ya Sudan dhidi ya FC Lupopo mchezo utakaochezwa
siku ya Jumapili nchini Sudan.
Mwamuzi Israel Mujuni
akisaidiwa Frank Komba na Soud Lila, mwamuzi wa akiba akiwa ni Mfaume
Ali Nassoro katika mchezo kati ya Renaissance Football Club (Chad) v
E.S.T. (Tunisia) wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) nchini Chad.
Mchezo namba 97 wa kuwania
kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kati ya Lesotho v
Shelisheli Machi 29, 2016 utachezeshwa na Israel Mujuni akisaidiwa na
Ferdinand Chacha, Samuel Mpenzu huku mwamuzi wa akiba akiwa Waziri
Sheha.
Mwamuzi Mfaume Ali Nassoro
atachezesha mchezo kati ya Burundi v Congo DR kuwania kufuzu kwa Fainali
za Mataifa Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20), Aprili
4, 2016 mjini Bunjumbura akisaidiwa na Frank John Komba, Alli Kinduli,
huku Martin Eliphas Saanya akiwa mwamuzi wa akiba


0 comments :
Post a Comment