Nkupamah media:
Waziri wa TAMISEMI George
Simbachawene akizungumza jana katika Mkutano wa nane wa wadau wa LAPF
unaoendelea jijini Arusha katika ukumbi wa AICC ambapo alikuwa mgeni
rasmi mbali na mambo mengine,aliitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa
mafao kwa wakati pindi wanachama wake wanapostaafu ili kuhakikisha kuwa
wastaafu wanapata mafao yao, kwani wengi wao wanakabiliwa na msongo wa
mawazo kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili baada ya kustaafu
wanashindwa kujimudu kutokana na kukosa mafao yao(Habari Picha na Pamela
Mollel wa jamiiblog Arusha)
Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama ameitaka mifuko ya
hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuunga mkono msimamo wa
serikali kuanzisha uchumi wa viwanda utakaotengeneza ajira na kuchochea
maendeleo ya nchi
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa
pensheni wa LAPF Eliudi Sanga akizungumza katika mkutano huo ambapo
alisema kuwa Mifuko ya hifadhi ya jamii imekua chachu ya maendeleo ya
taifa kutokana na uwekezaji unaofanywa na mifuko hiyo pamoja na mikopo
mbalimbali inayotolewa kwa wanachama kujikwamua kimaisha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha
Afisa Masoko wa LPF James Mlowe
akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa tayari mfuko huo
umeanzisha mkopo wa maisha popote na LAPF ambao unalenga kuwasaidia
watumishi wa umma hususan wale walioajiriwa maeneo ya vijijini ili
waweze kuanza maisha na kuwatumikia watanzania bila vikwazo vya
kiuchumi…
Makamu mwenyekiti wa bodi
Husein Kamote alisema mfuko huo unakabiliwa na changamoto nyingi
zinazokwamisha utekelezaji wa mipango yake ikiwemo deni inalolidai
serikali ambalo halijalipwa kwa mda mrefu huku likizidi kuongezeka
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akiteta jambo na Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga
Wadau katika mkutano
Mdau kutoka benki ya NMB akizungumza katika mkutano huo
Mwandishi wa habari wa star tv Ramadhan Mvungi akifatilia mkutano kwa ukaribu
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo
Waziri wa TAMISEMI George
Simbachaweneakimkabidhi kaimu mkurugenzi Geita John Muta hundi ya
shilingi milioni saba tu baada ya halmashauri hiyo kufanya vizuri na
mfuko huo
Wadau wakifatilia mkutano
Wadau kutoka mifuko mingine pia walishiriki mkutano huo
Mnufaika wa LAPF kupitia maisha
popote Scolastika Francis kutoka Kilolo ambaye ni mwalimu akitoa
ushuhuda jinsi mkopo huo ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo sasa
anamiliki nyumba pamoja na shamba mbali na ajira yake
Mwalimu wa shule ya
sekondari Rombo Njuguna Rombo akitoa ushuhuda jin si mfuko huo
ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo ameweza kununua


0 comments :
Post a Comment