Nkupamah media:
Meneja
wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, akizungumza na
waandishi wa Habari walipotembelea mradi wa viwanja vya mikopo
vinavyotolewa na taasisi yao, katika eneo la Kimara Ng’ombe, Bagamoyo,
mkoani Pwani jana. Picha zote na Mpiga Picha Wetu, Bagamoyo.
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
WAKAZI
na wananchi wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, wamepokea vizuri mradi wa
viwanja vya mikopo vinavyotolewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport
Financial Services, wakisema kuwa mradi huo utachangia kwa kiasi kikubwa
kuupanua na kuuweka mji wao katika kiwango cha juu kimaendeleo.
Meneja
wa Bayport Financial Services wilayani Bagamoyo Francis Ndunguru
akionyesha alama za viwanja vilivyopimwa katika eneo la mradi wa Kimara
Ng’ombe, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinauzwa kwa
mkopo kwa watu wote wenye kuhitaji kumiliki ardhi.
Kwa mjini Bagamoyo, mradi huo wa viwanja vya Bayport unapatikana Kimara
NG’ombe, huku maeneo mengine ya nchi viwanja hivyo vikipatikana KIbaha,
Chalinze, Morogoro, Kilwa na KIgamboni, vikihusisha watumishi wa umma,
wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.
NG’ombe, huku maeneo mengine ya nchi viwanja hivyo vikipatikana KIbaha,
Chalinze, Morogoro, Kilwa na KIgamboni, vikihusisha watumishi wa umma,
wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.
Meneja akionyesha barabara zilivyochongwa kuonyesha ubora wa mradi huo wa Bagamoyo, mkoani Pwani.
Mwandishi
wa habari Phillip Daud, akimhoji mwananchi wa Bagamoyo, Mwanaisha
Khalfany juu ya ubora wa viwanja hivyo na uwezekano wa Watanzania
hususan wakazi wa Bagamoyo kuvichangakia viwanja hivyo vilivyopimwa na
vyenye hati.
Akizungumza
na mtandao huu, mkazi wa Bagamoyo, Said Juma, alisema kwamba huduma za
viwanja vya Bayport vinavyopatikana kwa fedha taslimu na mikopo si vya
kukosa, kwa sababu zitachangia kuuweka mji wa Bagamoyo kwenye kiwango
cha juu pamoja na kujibu malalamiko ya wananchi kushindwa kumiliki
viwanja kwa njia rahisi na isiyokuwa na gharama kubwa.
“Uwezekano wa kumiliki viwanja
Bagamoyo mjini ni mgumu kwa sababu vinauzwa bei ghari, hivyo kwa Bayport
kuanzisha huduma hizi kwa watu wote bila kusahau sisi wajasiriamali,
hakika ni jambo la kushukuru na kuwapongeza kwa mawazo yao mazuri yenye
kutuendeleza sisi wananchi na wateja wao,” alisema Juma na kuwataka watu
wa Bagamoyo na Watanzania wote kuchangamkia fursa hizo.
Mwananchi mwingine aliyekutwa
kwenye mradi huo, Bi Mwanaisha Khalfany Sultan, alisema kwa kuanzisha
mradi huo wa viwanja mji wao wa Bagamoyo utapanuka na kuongeza idadi ya
watu wilayani humo.
“Tunafurahia kwa kiasi kikubwa
mno kupata mradi huu wa mikopo ya viwanja vya Bayport tukiamini mji wetu
utapiga hatua kubwa, hivyo tunawaomba kila mwenye uwezo wake na hitaji
la kujenga achangamkie fursa hii muhimu kwa Watanzania wote, ukizingatia
kuwa rasilimali ya ardhi ni muhimu na imekuwa ikiongezeka thamani kwa
haraka nchini kote, huku katika eneo la mradi wa Kimara Ng’ombe mahitaji
ya maji, umeme na barabara yakipatikana kwa urahisi,” alisema
Mwanaisha.
Naye mwananchi Patrick Mwilongo,
aligusia ubora wa mradi wa viwanja vya Kimara Ng’ombe akisema kuwa
utakuwa umejibu swali na malalamiko ya wanasiasa waliokuwa hawataki
Bagamoyo iingie kwenye Mamlaka ya Mji mdogo kwa madai kuwa mji utakuwa
mdogo, ukizingatia kuwa endapo eneo hilo litajengwa mji huo utakuwa
mkubwa na utapiga hatua kubwa kimaendeleo.
“Ni miongoni mwa wadau muhimu wa
hapa Bagamoyo ambao hakika tumeendelea kuthamani mradi huu kwa sababu
utakuwa na tija kwetu sote, hivyo ni wazi tunapaswa kujitokeza kupata
viwanja hivi ili tujenge kwa sababu uwezo wa kununua kiwanja kwa fedha
taslimu kwa baadhi yetu ni mgumu, ukizingatia kwa masharti nafuu unaweza
kupata kiwanja kwa kukopeshwa na Bayport.
Naye Meneja wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, alisema kwamba lengo ni kusudio lao kuu kuona mji wa Bagamoyo unakuwa na wananchi wanamiliki viwanja hivyo kwa utaratibu rahisi, hivyo ni budi kutembelea kwenye tawi lao la MJini Bagamoyo pamoja na matawi yote Tanzania ili kupata viwanja hivyo kwa ajili ya kuweka makazi ya kifamilia, kibiashara na mengineyo.
Naye Meneja wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, alisema kwamba lengo ni kusudio lao kuu kuona mji wa Bagamoyo unakuwa na wananchi wanamiliki viwanja hivyo kwa utaratibu rahisi, hivyo ni budi kutembelea kwenye tawi lao la MJini Bagamoyo pamoja na matawi yote Tanzania ili kupata viwanja hivyo kwa ajili ya kuweka makazi ya kifamilia, kibiashara na mengineyo.
“Tunawaomba Watanzania wote
popote walipo kutembelea ofisi zetu au mawakala wetu walionea nchi nzima
ili wapate fursa ya kukopa viwanja hivi kwa mji wa Bagamoyo au
vilivyopo kwenye maeneo mengine ya Tanzania, tukiamini Bayport
imeendelea kuwa mkombozi wa watu wote kwa kumiliki kiwanja kwa utaratibu
rahisi,” alisema Ndunguru, Meneja wa Bayport Bagamoyo.
Mita Moja ya mraba kwa viwanja
vya Bagamoyo inapatikana kwa Sh 10,000, Kigamboni (Tundi Songani) Sh
10,000, Kibaha (Boko Timiza) Sh 9000, Kilwa (Msakasa) Sh 2000, Morogoro
(Kiegea B) Sh 3500, Chalinze (Kibiki na Mpera) Sh 4500 tu, huku
utaratibu wa kuweza kupata viwanja hivyo ukiwa rahisi kwa Watanzania
wote, wakiwamo waaajiriwa wa serikali, waajiriwa binafsi na
wajasiriamali.


0 comments :
Post a Comment