-Naibu Waziri awakumbusha wanufaika kurejesha mikopo
Viongozi
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Jumuiya ya
Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) wamekutana mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki ili kubadilishana mawazo na kukubaliana kuendeleza
ushirikiano ili kutatua kero za wanafunzi.
Katika
mkutano huo, uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu John, wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa TAHLISO kutoka taasisi za elimu ya juu nchini
wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bw. Peter Kadugalize walikutana kwa siku
nzima na viongozi wa HESLB walioongozwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
HESLB Bw. Jerry Sabi na kujadiliana njia bora za kutatua kero za
wanafunzi.
Akizungumza
katika mkutano huo, Bw. Kadugalize aliiomba HESLB kuhakikisha Mameneja
wa kanda wa HESLB waliopo katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Mwanza, Mbeya
na Zanzibar wanatembelea vyuo vilivyopo katika maeneo yao na kukutana na
viongzi wa Serikali za wanafunzi kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua
kero zao.
“Tunaomba
hawa Mameneja wa Kanda washirikiane nasi kwa kuja vyuoni na kukutana na
sisi…kero nyingi za wanafunzi zinaweza kutatuliwa kwa njia hiyo badala
na kurundikana hadi tukutane na viongozi wa wakuu wa Dar es Salaam,”
alisema Bw. Kadugalize.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) Bw. Jerry Sabi akiongea na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya
Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) uliofanyika mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TAHLISO Bw. Stanslaus
Kadugalize. (Picha na HESLB).
Kuhusu
changamoto zinazowakabili vyuoni, Bw. Kadugalize alizitaja baadhi ya
kero kuwa ni pamoja uelewa mdogo wa baadhi ya wanafunzi kuhusu sifa za
kupata mikopo inayotolewa na HESLB hususan wale wanaokata rufaa baada ya
kukosa katika maombi yao ya kawaida.
Akizungumzia
katika mkutano huo, Bw. Sabi, ambaye aliteuliwa na Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufunzi mwezi Februari mwaka huu kushika nafasi
hiyo, alisema ushirikiano katika ya HESLB na TAHLISO ni muhimu na
kuahidi kuuendeleza.
“Ushirikiano
huu ni muhimu, ndiyo maana tumekubali mimi na timu yangu kuja
kuwasilikiza na kuwapa majibu ya maswali yenu,” aisema Bw. Sabi.
Akifafanua
kuhusu sifa za waombaji mikopo, Bw. Sabi alisema sifa na vigezo
hutolewa kila mwaka na kuwasihi waombaji wote wa mikopo kusoma kwa
makini na kuzingatia sifa hizo kabla ya kuomba mikopo.
“Ninawasihi
msome kwa makini sifa na vigezo kabla ya kuomba…kuhusu rufaa, ni muhimu
kila mwombaji anayekata rufaa kuthibitisha uhitaji wake kwa
kuaambatanisha nyaraka muhimu zinazohitajika na ambazo zimethibitishwa
na mamlaka husika…bila hivyo sisi tutashindwa kuthibitisha,” alisema Bw.
Sabi katika mkutano huo.
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu
(TAHLISO) kutoka Chuo Kikuu cha Bugando Bw. Elia Kandonga akiongea
katika mkutano kati ya TAHLISO na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu
ya Juu (HESLB) na kufanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Wakati huohuo,
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi,, Teknolojia na Ufunzi Mhandisi Stella
Manyanya amewataka wahitimu wa vyuo vikuu ambao ni wanufaika wa mikopo
ya elimu ya juu inayotolewa na HESLB kuhakikisha warejesha mikopo hiyo.
Akizungumza
katika hafla ya kuwapongeza wahitimu wa mwaka 2015 kutoka katika
taasisi za elimu ya juu nchini waliofanya vizuri katika masomo yao
iliyoandaliwana TAHLISO, Naibu Waziri watanzania wengi wanahitaji mikopo
ya elimu ya elimu ya juu na hivyo ni muhimu fedha hizo zikarejeshwa ili
ziwanufaishe wengine.
“Kuna
wengi wanaohitaji na bajeti ni finyu, ni vema mkarejesha ili
ziwanufaishe wengine…na wazazi wahakikishe vijana wao waliopata elimu
kwa nia ya mikopo wanaanza kurejesha,” alisema Naibu Waziri katika hafla
iliyofanyika katika ukumbi wa Mt. Gaspar mjini Dodoma mwishoni mwa wiki
na kuhudhuriwa na watendaji kutoka HESLB, Tume ya Vyuo Vikuu (TCU),
wazazi na wanafunzi.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Bw. Jerry Sabi
alisema hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu, jumla ya shilingi 2.3
trilioni zilikuwa zimetolewa kama mikopo ya elimu ya juu kwa watanzania
wahitaji na kuwa Bodi imeanza kutekeleza mikakati mbalimbali ili
kurejesha mikopo iliyoiva.
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu
(TAHLISO) kutoka vyuo mbalimbali nchini katika picha ya kumbukumbu na
viongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
waliokutana katika Chuo Kikuu cha Mt. John mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki.
Mikakati
hiyo ni pamoja na kuwashirikiasha watendaji wakuu wa serikali wakiwemo
Katibu Mkuu – Hazina na Msajili wa Hazina ambao wamewaelekeza waajiri
wote serikalini kuihakikisha wanufaika wote wa mikopo wanarejesha
mikopo.
Makakati
mwingine ni kuingia mkataba na Kampuni ya CreditInfo Tanzania Ltd ambao
utaziwezesha taasisi za fedha nchini kuwabaini wanufaika wa mikopo ya
elimu ya ju kabla ya kuwakopesha pale wanapokwenda katika taasisi hizo
kwa ajili ya kukopa fedha.
HESLB
ilianzishwa kwa sheria ya Bunge mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi
Julai 2005 kwa lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi watanzania wahitaji
waliopata nafasi ya kusoma katika vyuo vikuu. Aidha, HESLB ina jukumu la
kukusanya madeni yote ya mikopo ya elimu ya juu iliyotolewa na Serikali
tangu mwaka 1994/1995.
Baadhi
ya wahitimu bora wa vyuo vikuu mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandishi Stella Manyanya katika
hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu
(TAHLISO) ili kuwapongeza na kufanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
(Picha HESLB).


0 comments :
Post a Comment