Timu ya watu 16 imeundwa ili kuhakiki upya watumishi hewa katika halmashauri zote mkoani Mbeya, lengo likiwa ni kujiridhisha.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema kwenye uzinduzi wa mradi wa
uimarishaji mifumo ya sekta za umma kutokana na kuwapo kwa tatizo la
watumishi hewa.
“Rais alituagiza kuhakiki watumishi wote na
ikafanyika hivyo, lakini kutokana na kuwapo kwa udanganyifu nimeunda
timu ambayo imeanza kazi jana (juzi) kuhakiki upya watumishi ili
kujiridhisha na kupata ukweli wa watumishi wetu,” amesema.
Makalla
amesema timu hiyo imegawanyika katika makundi mawili na kwamba, wajumbe
wanatoka idara mbalimbali za Serikali wakiwamo wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru)



0 comments :
Post a Comment