Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi kubwa ya Chama Cha Skauti wa
Kike nchini hivi sasa ni kuhakikisha kinarejesha heshima ya mwanamke
katika jamii.
Samia ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofika ofisi kwake Ikulu kwa ajili ya kuelezea shughuli zao katika kusaidia watoto wa kike waweze kujitambua na hatimaye kulitumikia Taifa.
Alisema
pamoja na chama hicho kinafundisha kujenga ujasiri na kuwa huru kwa
mtoto wa kike lakini kuna haja ya kukumbushana umuhimu wa kuzingatia
mila na desturi nzuri zilizopo katika matendo yao ili kurejesha heshima
ya mwanamke.
"Sasa
hivi utakuta binti kavaa kipanti kinambana hasa, anazunguka barabarani
huku na kule, mwenyewe anajiona yuko sawa...hicho ni kinyume kabisa na
maadili yetu, mila na desturi zetu za kiafrika tumeziacha kabisa."
alisema Makamu wa Rais.
Aidha
alisema katika enzi hizi za utandawazi kumekuwa na urushwaji wa mambo
yasiyo na maadili katika mitandao jambo ambalo mtoto wa kike anaweza
kuutumia uhuru huo kwa kufanya mambo kinyume na mila na desturi.
Alisema
pamoja na kwamba Tanzania inapingwa na mataifa makubwa kwa kupitisha
sheria ya makosa ya mtandao lakini bado chama hicho kina kazi kubwa ya
kusaidia jitihada za serikali katika kulea watoto wa kike kimaadili.
"Nyinyi
Girl Guide mna hiyo kazi ya kusaidia kuwalea watoto wa kike
waliojengeka vizuri kimaadili na wanazingatia mila na desturi,"
alidokeza Samia
Makamu
wa Rais alikitaka chama hicho pia kuandaa miradi kwa ajili ya kusaidia
ujenzi wa vyoo bora mashuleni kulingana na mahitaji ya watoto wa kike na
hivyo kuwawezesha kuhudhuria masomo siku zote bila kukosa kama ilivyo
kwa wavulana.
Mwenyekiti
wa chama hicho, Matilda Balawa alimshukuru Makamu wa Rais kwa kukubali
kuwa mwanachama na kupongeza utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano chini
ya Rais John Magufuli.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na
Wanachama wa SKAUT Nchini.Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
katika picha ya pamoja na Wanachama wa SKAUT Nchini.
Makamu wa Rais Mhe. Samia akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Baraza la TAWLA






0 comments :
Post a Comment