Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe, (katikati) pamoja na ujumbe
wake wakifanya ukaguzi wa kushitukiza katika mgodi wa Kiwanda cha
Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd , katika mgodi wa
Kiwanda hicho uliopo eneo la Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu,
Kata ya Gwata, Tarafa ya Mikese, wilaya ya Morogoro, kiwanda hicho
kinamilikiwa na wachina, uzalishaji wake ulizuiwa na Serikali kuu
tangu mwaka 2010 hadi watakapokamilisha taratibu zote za kisheria
zikiwemo na za kimazingira.
Mfanyakazi
raia wa China, Wang Jun (33) ambaye ni mtunza stoo katika mgodi wa
kutengeneza marumaru wa Kiwanda cha Tanzania Zhong Fa Construction
Material Group Co Ltd ,kinachomilikiwa na Wachina akiwa chini ya ulinzi
wa Polisi kufuatia ukaguzi wa ghafla wa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk
Kebwe Steven Kebwe, Aprili 13,2016 akifuatana na ujumbe wa serikali ya
mkoa na wilaya ya Morogoro katika mgodi wa Kiwanda hicho uliopo
Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Tarafa ya Mikese
, ambapo walikutwa wakiendelea na uzalishaji licha kuzuiwa na Serikali
kuu mwaka 2010 hadi watakapokuwa wamekamilisha taratibu zote za kisheria
zikiwemo na za kimazingira.
Na John Nditi, Morogoro
RAIA
wawili wa China wametiwa nguvuni mkoani Morogoro kutokana na kuendelea
kusimamia shughuli za uzalishaji wa marumaru katika mgodi wa mawe wa
Kiwanda cha Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd ,kinachomilikiwa
na Wachina licha ya kuzuiwa na Serikali kuu tangu mwaka 2010.
Mbali
na kuendelea na uzalishaji katika kipindi chote hicho, kampuni hiyo
imekuwa ikifanya udangayifu kuwa marumaru zinazouzwa katika maduka
yake zinaingizwa kutoka nchini China , wakati bidhaa hiyo ikitengenezwa
kutoka Morogoro.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe, aliamuru kukamatwa kwa raia
hao baada ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza Aprili 13, 2016 akiwa
na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na viongozi wa
halmashauri ya wilaya ya Morogoro.
Kampuni
hiyo ilizuiwa kuendelea na uzalishaji wa marumaru katika mgodi uliopo
katika Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Tarafa
ya Mikese tangu Novemba 30, mwaka 2010 , lakini imeendelea na
uzalishaji kwa kipindi chote hicho bila kuwa na vibali wala taratibu
zote za kisheria zikiwemo za hifadhi ya kimazingira.
Hatua
ya Mkuu kufanya ziara hiyo ni kwenda kujiridhisha kutokana na taarifa
ya uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro iliyowasilisha
vielelezo mbalimbali juu ya kampuni hiyo kushindwa kulipa tozo la
kiasi cha Sh milioni sita kwa hesabu za wakati huo kabla ya kuzuiwa na
Serikali.
Dk
Kebwe alisema, licha ya kuzuiwa na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo ,wakati wa Serikali ya awamu ya nne kabla ya
mabadiriko ya wizara hiyo baada ya Waziri kutembelea mgodi huo na
kukuta wakiendesha uzalishaji bila kuwa na leseni na vibari kutoka
katika mamkala mbalimbali ikiwemo ya wizara hiyo .
“
Tangu wakati wa Waziri Profesa Muhongo awamu ya kwanza walipozuiwa
kuendea na uchimbaji hadi watakapo kamilisha utaratibu wa kisheria
zikiwemo na za hifadhi ya kimazingira, wameendelea kuzalisha katika
mgodi bubu ...wamechimba eneo na kurivuruga kimazingira “ alisema Mkuu
wa Mkoa Dk Kebwe.
Dk
Kebwe alisema , uzalishaji wa marumaru katika mgodi huo umekuwa
ikiendelea kwa njia zisizo halali ambapo bidhaa hiyo inatengezwa eneo
hilo na kusafirishwa katika maduka ya Kampuni hiyo yaliyopo Jijini
Arusha na Dar es Salaam kwa ajili ya kuuzwa ndani na nje ya nchi.
“
Ufuatiliaji umekuwa ukifanyika mara kwa mara eneo la mgodi na uzalishaji
umekuwa ukifanyika kama tulivyowakuta hapa na marumaru hizi
zikifikishwa katika maduka hayo zinajazwa kwenye makadha yaliyoandikwa
kwa lugha ya kishina ya kampuni hii na kuonesha zimeingizwa kutoka China
na kuuzwa ka bei ghali “ alisema Dk Kebwe.
“
Tumenunua marumaru zilizo kwenye maduka haya na kubaini hazitoki China
bali ni Morogoro kwenye mgodi unaozalisha bidhaa hizi na kuwekwa nembo
ya Kichina kwa jina hilo la kampuni ...huu ni wizi na kuikosesha
serikali na halmashauri mapato yake” alisisitiza Mkuu wa mkoa , Dk
Kebwe.
Mkuu
wa mkoa , Dk Kebwe alisema , tangu mwaka 2010 walipozuiwa na Serikali
kupitia Wizara ya Nishati na Madini, uzalishaji umeendelea kukua katika
mgodi huo ambapo marumaru hizo kwa sasa zinasafirishwa kuuzwa katika
nchi jirani za Afrika Mashariki na Kati zikiwa na lebo ya kutoka nchini
China.
“
Kutokana na udanganyifu na wizi unaofanyika ndiyo maana kiwanda hiki
hakijafungua Duka hapa Morogoro isipokuwa ni Dar es Salaam na Arusha ili
watanzania wajue ni bidhaa kutoka China , na bei ya chini ya marumaru
moja ndogo ni Sh 280,000 , jambo hilo lazima tulikomeshwe “ alisema Dk
Kebwe.
Pia
Dk Kebwe aliitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Morogoro
kuanza mara moja kufanya tathimini ya mauzo ya marumaru zinazotokana na
uzalishaji wa mgodi huo ili kupata mauzo halisi ya Kampuni ili
kuiwezesha halmashauri kupata malipo ya halali .
Kutokana
na kukaidi agizo la Serikali , mkuu wa mkoa Dk Kebwe aliamuru kukamatwa
kwa wafanyakazi wawili wa China wa Kiwanda cha Zhong Fa Construction
Material Group Co Ltd na msimamizi wa kitanzania kwa lengo la
kuisaidia serikali ya mkoa katika uchunguzi wake juu ya kiwanda
hicho.
Wachina
waliokamatwa na Polisi eneo la mgodi ni Mtunza stoo Wang Jun (33) na
mwezake Shiqing Liang (36) ,wakati mtanzania ni Hilary Paulo.
Naye
Ofisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Bertha Luzabiko, alimwezeza
mkuu wa mkoa kuwa licha ya kuhamia mkoa huo mnamo Novemba mwaka 2014 ,
kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kushughulikia maombi ya Kampuni hiyo ,
lakini iligundulika kuwa eneo hilo tayari lina leseni ya mwekezaji
mwingine na si rahisi kutolewa nyingine.
Luzabiko
alisema aliwaadikia barua wenye mgodi huo ya kuwasimamisha
kuendelea na kutokana na eneo hilo lina leseni ya mtu mwingine wa
uchimbaji wa dhahabu.
Hivyo
alisema baada ya kuwandikia barua ya kusitisha shughuli zao , aliamua
kufanya mara tatu kwa nyakati tofauti alikuta shughuli uchimbaji na
utengenezaji wa marumaru ukiendelea , ndipo alipoamua kuripoti Polisi
ili watu hao wakamatwe na kufunguliwa kesi mahakamani zoezi ambalo
lilifanyika.
Lizabiko
alisema, licha ya kukamatwa kwao, bado waliendelea na uzalaishaji
ambapo pia aliamua kulifikisha suala hilo kwa Kamishina wa Madini
Kanda ya Mashariki aliyemtaja kwa jina la Hamis Komba ili kuchukua
hatua za kisheria na kiutawala.
Naye
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mkoa wa Morogoro Philip
Kimune , aliyefuatana na Mkuu wa mkoa eneo la mgodi huo alisema taarifa
zilizipo kwenye Mamkala ya Mapato zinaonesha kuwa , kampuni hiyo
inatumia jina la Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd.
Alisema
,kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011 hadi Machi 2016 kiwanda hicho
kilionesha kuwa mauzo ya kiasi cha Sh bilioni 30.9 yaliyolipiwa Vat
ya Sh bilioni 5.5.
Mbali
na hayo alisema , mauzo hayo hayakuonesha iwapo yalitokana na bidhaa
ya marumaru ama yalijumuishwa na bidhaa nyinginezo zinazozalishwa na
kampuni hiyo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Yona Maki alisema ,
kuchelewa kwa mchakato wa kukusanya ushuru katika kiwanda cha
kuchoronga mawe cha wachina kinaikoseha mapato halmashauri kiasi cha
zaidi ya Sh milioni 90 kwa kipindi cha miaka sita kuanzia mwaka 2010.
Sehemu ya Muonekano wa Kiwanda hicho.
Mfanyakazi wa Mgodi huo, Hilary Paulo (kulia) akimpatia maelezo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe.
0 comments :
Post a Comment