Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akipokea maua kutoka
kwa mtoto Sharon Innocencia Shiyo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya
Ikulu jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya
Muungano Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika viwanja
vya Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili
ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akikagua Gwaride la
Heshima mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akiwa amesimama na
Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akitia
saini kwenye mkataba wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa
Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akitia saini kwenye
Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli
akibadilishana makabrasha ya mkataba na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Mayardit mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji Saini wa kuiwezesha
Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit kabla ya utiaji saini wa
Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais Dkt. Magufuli akitoa hotuba yake mara baada ya zoezi la
utiaji Saini kukamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mgeni wake Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit wakipiga makofi mara
baada ya kufurahishwa na wimbo wa bendi ya Polisi iliyokuwa ikitumbuiza Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit
pamoja na viongozi wengine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan watatu
kutoka kushoto na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa watatu kutoka kulia.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia wakati Bendi ya
Matarumbeita ilipokuwa ikitumbuza Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.
0 comments :
Post a Comment