Mrema Ajitokeza Kwa Mara Nyingine Tena Kumkumbusha Rais Magufuli Ampe Kazi Yoyote


Mwenyekiti wa TLP taifa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema amesisistiza ombi lake la kazi kwa kumkumbusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwamba ampe kazi yoyote amsaidie kibarua kigumu alichonacho cha kuwahudumia wananchi

Dkt. Mrema ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu miaka 32 ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine ambaye alihudumu kwenye awamu ya kwanza ya Mwl. Julius Nyerere ambapo alifariki akiwa na cheo cha waziri mkuu tarehe 12.04.1984 kwa ajali ya gari.

''Namkumbuka Sokoine kama mtu wa watu aliyehudumia watu,aliyepambana na ufisadi na magendo .Alikuwa anatenda haki kwa wananchi wote .

"Hata mimi nilipokuwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu nilijaribu kufanya kama yeye bahati mbaya sikufanikiwa kama yeye kwa sababu sikuwa waziri mkuu au Rais''- Alisisistiza Mrema.

Kuhusu Mrema kuomba kazi kwa Dkt. Magufuli 
Mrema alisema kwa kutambua rekodi yake ya utendaji kazi wa  Rais Dkt. Magufuli, aliwahimiza wananchi wa Vunjo wamchague kipindi cha kampeni na yeye akampigia kampeni na Rais akawaambia wananchi wa Vunjo kwamba Mrema akikosa ubunge atapangiwa kazi nyingine ndiyo hiyo wananchi wanaulizia.

Aidha Mrema alisema kuna maeneo ambayo yeye anafiti siyo lazima apewe madaraka makubwa 

"Mimi sihitaji ukuu wa mkoa au uwaziri, anipe kazi yoyote na nikionana naye nitamkonyeza maeneo ambayo ninafiti ili nimsaidie kutumbua majipu." Alisema Mrema

Hata hivyo Dkt. Mrema alimpongeza Dkt. Magufuli kwamba ni mtendaji ambaye ameamua bila kusukumwa kupambana na mafisadi na kwamba yeye ni alfa na omega na kazi hiyo ameonyesha kwamba atafanya vizuri kuliko Sokoine na Mrema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment