Rais Rousseff amelaani hatua hiyo na kuitaja kuwa mapinduzi ya kisiasa.
Kamati ya bunge nchini Brazil imeidhinisha hatua ya kumuondoa madarakani Rais Dilma Rousseff, na kutoa fursa ya kupigwa kura baadaye wiki hii kuamua ikiwa ataondolewa ofisini.
Baada ya mjadala mkali, kamati hiyo ilipiga kura kwa asilimia 38 kwa 27 na kupitisha kuondolewa kwake madarakani.
Rais Rossef anakana madai ya kuvuruga akaunti za serikali ili kuficha kudorora kwa uchumi.
Amelaani hatua hiyo na kuitaja kuwa mapinduzi ya kisiaia. Shughuli za Rais zimehujumiwa na uchumi unaozidi kuzorota pamoja na sakata kubwa ya ufisadi inayoikumba kampuni ya mafuta ya serikali Petrobras.
Chanzo:BBC
0 comments :
Post a Comment