Klabu
ya Simba SC ya jijini Dar es salaam (Pichani) imethibitisha kushiriki
michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itakayoanza
kutumia vumbi Mei 22, 2016 nchini Sudan.
Mashindano
ya vilabu Kombe la Nile Basin huandailiwa na CECAFA kwa kushirikisha
vilabu vilivyoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi kwa nchi
wanachama wa CECAFA.
Bingwa
michuano ya kombe hilo atajinyakulia zawadi ya dola za kimarekani
U$30,000, mshindi wa pili dola U$20,000, huku mshindi wa tatu akipata
kitita cha dola za kimarekani U$10,000.
Nile
Basin inashirikisha vilabu kutoka katika nchi wanachama wa CECAFA ambazo
ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania na
Zanzibar.
Vitoria
University kutoka Uganda ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya
kuifunga AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali
uliofanyika mwaka 2014.
0 comments :
Post a Comment