Golikipa wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegan amekanusha uvumi ulikuwa umesambaa kuwa amesaini mkataba na Manchester City na kueleza atazungumza hatma yake baada ya msimu kumalizika.
Akizungumza na kituo cha redio cha Al Primer Toque alisema hakuna dili lolote na Mnchester City nakwa sasa anachoangalia ni kucheza vizuri na kuona timu yake ikishinda michezo yake.
“Sio kweli kuwa nimesaini Manchester City … mwishoni kwa msimu tutaangalia hali jinsi ilivyo ndipo nitazungumza tena, sawa? Tuna michezo mingi kwa sasa na hilo ndiyo pekee naweza kusema kwa sasa,
“Kwa mimi jambo muhimu ni kucheza vyema na tushinde michezo yetu yote. Barcelona ni timu kubwa, siwezi kusema zaidi, tutaona jinsi itakuwa,” alisema